Ajira Tanzania

Ajira Mpya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mei 2025

Ajira Mpya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mei 2025

NAFASI Za Kazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilianzishwa rasmi kupitia Tangazo la Rais kuhusu mgawanyo wa majukumu ya Wizara (GN. No. 534) lililotolewa tarehe 2 Julai, 2021. Wizara hii ina jukumu la kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sera zinazohusu masuala ya mambo ya nje, ushirikiano wa kimataifa na ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Majukumu ya wizara pia yanahusisha usimamizi wa ushirikiano wa pande mbili na pande nyingi, uratibu wa mikataba ya kimataifa, makubaliano, diplomasia ya kiuchumi, masuala ya diaspora, huduma za kibalozi na uboreshaji wa utendaji na rasilimali watu.

Nafasi ya Kazi: Foreign Service Officer – Nafasi 12

Majukumu ya Kazi

  • Kuandaa ajenda, kumbukumbu na taarifa za vikao vya kimataifa
  • Kushiriki mikutano ya kitaifa na kimataifa na kuandika ripoti
  • Kuandaa taarifa za viongozi wa kitaifa kwa ajili ya mikutano ya pande mbili, mikutano ya kimataifa, mahojiano n.k.
  • Kufuatilia masuala ya kimataifa, kufanya uchambuzi na kutoa ushauri
  • Kufanya tafiti kuhusu masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa na kutoa mapendekezo
  • Kutunza kumbukumbu za matukio mbalimbali ya kidiplomasia na matukio ya kimataifa
  • Kutekeleza majukumu mengine atakayopangiwa na mkuu wake wa kazi

Sifa za Mwombaji

Mwombaji anatakiwa awe na Shahada ya Kwanza (Bachelor) katika mojawapo ya fani zifuatazo:

  • Mahusiano ya Kimataifa
  • Uchumi
  • Sheria
  • Sheria za Kimataifa
  • Usimamizi wa Biashara
  • Sayansi ya Siasa
  • Biashara ya Kimataifa
  • Sera za Umma
    Au sifa nyingine zinazolingana kutoka taasisi inayotambuliwa.

Mshahara

Ngazi ya mshahara: TGS D

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  • Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45 (isipokuwa walioko kwenye utumishi wa umma)
  • Watu wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na watambulishe hali yao kwenye mfumo wa maombi
  • Ambatanisha CV ya kisasa yenye mawasiliano sahihi (anuani, baruapepe, simu)
  • Ambatanisha nakala zilizothibitishwa za vyeti vya taaluma, kidato cha nne na sita, na vyeti vya usajili wa kitaaluma (kama inahitajika)
  • Vyeti vya matokeo (results slips), testimonials na partial transcripts havitakubalika
  • Pakia picha ndogo ya hivi karibuni (passport size) kwenye mfumo
  • Aliyewahi kustaafu katika utumishi wa umma haruhusiwi kuomba
  • Eleza majina ya waamuzi watatu wenye mawasiliano sahihi
  • Vyeti vya elimu kutoka nje ya nchi vihakikiwe na NECTA (kwa O/A level) na TCU/NACTE kwa vyuo vya elimu ya juu

Maelekezo ya Uwasilishaji wa Maombi

Barua ya maombi iwe imeandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza na ipelekwe kwa:

Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, S.L.P 2320, Dodoma
Majengo ya Utumishi, Chuo Kikuu cha Dodoma – Jengo la Dr. Asha Rose Migiro

Maombi yote yatumwe kupitia tovuti ya ajira:
👉 http://portal.ajira.go.tz

Maombi yaliyotumwa nje ya mfumo huo hayatapokelewa.

Mwisho wa Kupokea Maombi

🗓 Tarehe ya mwisho kutuma maombi ni 31 Mei, 2025

Angalizo: Watakaoitwa kwenye usaili ni wale tu waliopitia mchujo. Uwasilishaji wa vyeti vya kughushi utasababisha hatua za kisheria kuchukuliwa.

Leave a Comment