Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, amesema kuwa wachezaji wote wa kikosi cha Simba wapo tayari kuwatia moyo Wanasimba kwa msimu mpya. Msimu uliopita wa 2023/24, Simba ilimaliza ligi katika nafasi ya tatu baada ya mechi 30 na pointi 69, na itawakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na Coastal Union ya Tanga iliyomaliza katika nafasi ya nne.
Yanga, mabingwa wa ligi, na Azam FC waliomaliza nafasi ya pili, watashiriki kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Wachezaji muhimu ndani ya Simba ni pamoja na Deborah Fernandez, Edwin Balua, Mzamiru Yassin, Mohamed Hussein, Ayoub Lakred, Camara Mousa, na Kibu Dennis.
Ahmed Ally alisema, “Wachezaji wote wa Simba wapo tayari kwa msimu mpya wa 2024/25. Tunatambua kwamba msimu uliopita haukuwa mzuri kutokana na kutofikia malengo yetu, lakini tuna matumaini mapya na tunaanza kuyafikia.”
Agosti 8, 2024, itakuwa siku ya Kariakoo Dabi, ambapo Simba itakutana na Yanga katika Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Mkapa. Coastal Union itacheza dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, huku fainali ikifanyika Uwanja wa Mkapa.
Leave a Comment