Ahmed Ally Aeleza Mikakati ya Simba Day
Simba SC imejipanga kikamilifu kwa ajili ya Simba Day 2024 itakayofanyika katika Uwanja wa Mkapa, ikiwakutanisha na timu ya APR kutoka Rwanda kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa. Tukio hili litakuwa la kipekee kwani litahusisha utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwepo msimu uliopita wa 2023/24.
Hata hivyo, usajili wa Simba haujatikisa sana nchini kutokana na kuleta wachezaji wa kawaida ikilinganishwa na wapinzani wao wa jadi, Yanga. Yanga nao wanatarajia kutambulisha wachezaji wao na benchi la ufundi mnamo Agosti 4, 2024.
Mchezaji wa zamani wa Simba, Clatous Chama, aliyehamia Yanga, ni mmoja wa wachezaji wanaosubiriwa kwa hamu. Chama alifunga mabao saba na kutoa pasi sita za mabao msimu wa 2023/24. Mutale Joshua, ambaye ameng’ara katika kambi ya mazoezi ya Misri, pia anatarajiwa kufanya vizuri msimu huu.
Kambi ya mazoezi ya Simba huko Misri imekamilika na timu inatarajiwa kurejea nchini Julai 31 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea Simba Day. Tiketi za tukio hilo zinauzwa katika vituo mbalimbali.
Ahmed Ally Alivyojipanga Kutambulisha Wachezaji Simba Day
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, amesema kuwa maandalizi ya Simba Day yanakwenda vizuri na mashabiki wanapaswa kujitokeza kwa wingi. “Kila kitu kinakwenda vizuri kwa ajili ya Simba Day. Timu imeimarika baada ya kambi ya Misri na tunaamini itakuwa siku nzuri. Mashabiki wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Mkapa kwa burudani ya kweli.”
Kwa taarifa zaidi kuhusu maandalizi ya Simba Day, endelea kufuatilia habari kutoka Simba SC.
Leave a Comment