Audio

Komasava: Diamond Platnumz Aingia kwenye Billboard USA, Nafasi ya 39

Komasava: Diamond Platnumz Aingia kwenye Billboard USA, Nafasi ya 39

Diamond Platnumz Aingia kwenye Billboard USA na Komasava Remix

Msanii maarufu kutoka Afrika Mashariki, Diamond Platnumz, amefanya historia kwa mara ya kwanza kuingia kwenye chati za Billboard nchini Marekani. Hii ni baada ya wimbo wake, Komasava, kuorodheshwa kwenye nafasi ya 39.

Diamond alifanikiwa kupata nafasi hii baada ya kushirikiana katika remix ya wimbo huo na nyota wa Kanada, Jason Derulo. Remix hii imeongeza umaarufu wa wimbo, ukisaidia Komasava kuingia kwenye orodha ya ngoma za Afrobeats kwenye jukwaa maarufu la Billboard.

Katika orodha ya Billboard, wimbo wa Diamond umetambuliwa kwenye nafasi ya 39 kati ya ngoma 50 bora za Afrobeat. Taarifa hizi zinaonyesha jinsi Komasava ilivyopokelewa vyema kwenye majukwaa ya kutiririsha miziki, mauzo, na idadi ya vipakuliwa, pamoja na ushawishi wa wimbo huo kwa watazamaji nchini Marekani.

Diamond alishiriki taarifa hizi kwenye mitandao yake ya kijamii, akitoa wito kwa mashabiki wake kuongeza juhudi ili wimbo huo uweze kufika kwenye nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard.

“Ni wakati wetu kupeleka huu wimbo nambari moja, watu wangu,” alisisitiza Diamond.

Wimbo huu ulitolewa miezi minne iliyopita kwa ushirikiano na Chley na Khalil Harisson, ukipata zaidi ya milioni 4.8 za maoni kwenye YouTube hadi sasa. Remix ya wimbo huo, iliyotolewa siku 12 zilizopita na Jason Derulo, tayari imevutia zaidi ya milioni 7.8 za maoni kwenye YouTube.

Leave a Comment