Nafasi 107 za Kazi TARURA Mei 2025
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umefungua milango kwa Watanzania kuomba nafasi mpya 107 za ajira katika sekta ya uhandisi na ufundi. Nafasi hizi ni kwa Wahandisi wa Ujenzi (Civil Engineers) 50 na Mafundi wa Ujenzi (Civil Technicians) 57.
Kwa Wahandisi wa Ujenzi, majukumu ni pamoja na kuandaa michoro ya barabara, kufanya tafiti za kiuhandisi, kusimamia kandarasi za ujenzi, kuendesha mifumo ya usimamizi wa barabara, na kuhakikisha ubora wa miradi ya barabara unaendana na viwango. Waombaji lazima wawe na Shahada ya Uhandisi wa Ujenzi na wawe wamesajiliwa na Bodi ya Wahandisi (ERB).
👉 Bonyeza hapa kuomba nafasi ya Engineer (Civil) – 50 Posti
Kwa Mafundi wa Ujenzi, kazi zao ni pamoja na kushiriki katika ukarabati wa barabara, kufanya majaribio ya maabara, kusimamia kazi za ujenzi na kutoa taarifa za maendeleo ya miradi. Waombaji wanatakiwa kuwa na Stashahada au Cheti cha Ufundi Kamili (FTC) katika Ujenzi.
👉 Bonyeza hapa kuomba nafasi ya Technician (Civil) – 57 Posti
Maombi yanafungwa tarehe 31 Mei 2025, na yanapaswa kufanyika kupitia mfumo wa ajira wa serikali. Hii ni fursa muhimu kwa wataalamu wa sekta ya miundombinu kujiunga na taasisi yenye jukumu la kukuza maendeleo ya kiuchumi kupitia usimamizi bora wa mtandao wa barabara za vijijini na mijini.
Leave a Comment