Ajira Tanzania

Ajira Mpya Pangani District Council 2025

Ajira Mpya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani 2025 – Nafasi za Dereva na Uhazili

Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imetangaza nafasi mpya za ajira kwa mwaka wa fedha 2024/2025 baada ya kupata kibali rasmi kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Tangazo hili linatoa fursa kwa Watanzania wenye sifa kutuma maombi ya kazi kupitia mfumo rasmi wa Recruitment Portal kabla ya tarehe 02 Juni 2025.

πŸ”Ή 1. Nafasi za Dereva Daraja la II – Nafasi 7

Sifa za Mwombaji:

  • Awe na cheti cha Kidato cha Nne (Form IV)
  • Awe na leseni ya daraja E au C
  • Uzoefu wa kuendesha kwa mwaka 1 bila ajali
  • Awe na mafunzo ya msingi ya ufundi (VETA au chuo kinachotambuliwa)

Majukumu ya Kazi:

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari
  • Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi
  • Kufanya matengenezo madogo ya gari
  • Kusambaza nyaraka na kufanya usafi wa gari

Mshahara: Ngazi ya Serikali – TGS B

πŸ”Ή 2. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 5

Sifa za Mwombaji:

  • Cheti cha Form IV au Form VI
  • Diploma ya Uhazili au NTA Level 6
  • Uwezo wa hatimkato Kiswahili na Kiingereza (maneno 80 kwa dakika)
  • Uwezo wa kutumia kompyuta: Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher

Majukumu ya Kazi:

  • Kuchapa barua na nyaraka muhimu
  • Kupokea na kuelekeza wageni
  • Kusimamia majalada na maandalizi ya vikao
  • Kupanga dondoo na mahitaji ya vifaa

Mshahara: Ngazi ya Serikali – TGS C

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  • Raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45
  • Waambatanishe nakala za vyeti, CV, picha mbili za β€˜passport size’ na cheti cha kuzaliwa
  • Vyeti vya nje viwe vimehakikiwa na NECTA, NACTE au TCU
  • Walio kwenye ajira serikalini hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi

Jinsi ya Kutuma Maombi

Tuma maombi yako kupitia Recruitment Portal ya serikali:
πŸ‘‰ https://portal.ajira.go.tz

Anuani ya barua ya maombi:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani,
S.L.P 89,
PANGANI.

Usikose nafasi hii ya kipekee kujiunga na utumishi wa umma Pangani. Hakikisha umetuma maombi yako kabla ya tarehe 02 Juni 2025.

Leave a Comment