Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Utumishi Mei 19, 2025
Taarifa Muhimu Kwa Waombaji Kazi Waliowasilisha Maombi Serikalini
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametangaza rasmi orodha ya waombaji kazi walioitwa kwenye usaili wa taasisi mbalimbali za umma kuanzia tarehe 24 Mei hadi 28 Juni 2025. Usaili huu unahusisha waajiri kama OSHA, NIT, FCC, JKCI, TPDC, DUCE, DIT, NIRC, NACTVET, NSI, Makumbusho ya Taifa, Sekretarieti ya Maadili, MDAs & LGAs na wengine.
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa
Wasailiwa wote waliopata nafasi ya kuitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia masharti yafuatayo kabla ya siku ya usaili:
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe 24 Mei 2025, katika muda na eneo lililoainishwa kwa kada husika.
- Kila msailiwa anatakiwa kuvaa barakoa (mask) anapofika eneo la usaili.
- Wasailiwa wote wanapaswa kuja na kitambulisho halali kama vile cha NIDA, mpiga kura, kazi, uraia, leseni ya udereva au barua ya utambulisho ya serikali ya mtaa.
- Wajitokeze na vyeti halisi vya taaluma kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha nne na sita, stashahada, shahada n.k.
- Vyeti kama testimonials, provisional results au statement of results hazitakubalika.
- Wasailiwa watajigharamia usafiri, chakula na malazi.
- Taarifa sahihi kuhusu muda na sehemu ya usaili ipatikane kupitia akaunti binafsi ya Ajira Portal.
- Waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimeidhinishwa na NECTA, NACTVET au TCU.
- Kada zinazotakiwa kuwa na usajili maalum lazima zije na vyeti vya usajili pamoja na leseni ya kazi.
- Wasailiwa wenye tofauti ya majina katika nyaraka zao waje na Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa rasmi.
- Namba ya mtihani inapatikana kupitia akaunti ya Ajira Portal na haitatolewa siku ya usaili.
- Waombaji ambao hawajaona majina yao kwenye tangazo wanashauriwa kuingia kwenye akaunti zao na kuangalia sababu za kutokuitwa ili kuboresha nafasi zao kwa mizunguko ijayo.
Link ya Kupakua Majina ya Walioitwa
Pakua Orodha Kamili ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili hapa:
BONYEZA HAPA KUPAKUA PDF
Hitimisho
Huu ni mwito rasmi kwa waombaji waliokidhi vigezo, kuhakikisha wanajiandaa ipasavyo kwa ajili ya usaili. Kuwa makini na maelekezo yote ili usikose nafasi hii muhimu ya ajira serikalini.
Leave a Comment