Ajira Tanzania

Nafasi 4 za Customer Service Arusha – Ongeza Agrovet 2025

Nafasi 4 za Customer Service Arusha - Ongeza Agrovet 2025

Nafasi za Internship Ongeza Agrovet 2025 – Watoa Huduma kwa Wateja (4 Positions)

Fursa Mpya ya Mafunzo ya Kazi Ongeza Agrovet – Customer Service

Kampuni ya Ongeza Agrovet inatoa nafasi nne (4) za mafunzo ya kazi kwa vijana waliomaliza masomo yao, kwa nafasi ya Customer Service Interns. Ongeza Agrovet ni kampuni inayojikita katika kuboresha maisha ya wakulima na wafugaji kwa kuwapatia bidhaa na huduma bora za kilimo na ufugaji kote Tanzania. Kupitia teknolojia, ushauri, na upatikanaji wa bidhaa zenye viwango vya juu, kampuni hii inalenga kukuza kilimo endelevu na lishe bora vijijini.

Ikiwa na ushirikiano na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi, Ongeza Agrovet inapanua huduma zake kwa kasi ili kuchochea ukuaji wa sekta ya kilimo na mifugo kwa kutoa mbegu bora, dawa za mifugo, vifaa vya kisasa, pamoja na elimu kwa wakulima.

Nafasi Zinazotolewa: Customer Service – Internship (4 Nafasi)

Eneo: Arusha, Tanzania
Aina ya Nafasi: Mafunzo ya kazi (Internship)
Idadi ya Nafasi: 4

Vigezo vya Muombaji

  • Awe ni mhitimu mpya kutoka chuo kikuu au chuo cha kati
  • Awe na Diploma au Degree katika moja ya fani zifuatazo: huduma kwa wateja, mauzo na masoko, au uongozi wa biashara
  • Uwezo mzuri wa kuwasiliana na kuhudumia wateja
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa malengo na bila kusimamiwa kwa karibu
  • Uwezo wa kusikiliza na kutatua changamoto kwa haraka
  • Awe na ufasaha wa lugha ya Kiswahili na weledi wa lugha ya Kiingereza

Jinsi ya Kutuma Maombi

  • Tuma barua ya maombi pamoja na CV yako kwenye faili moja kwenda: [email protected]
  • Andika kichwa cha barua pepe kama ifuatavyo: CUSTOMER SERVICE INTERN
  • Mwisho wa kutuma maombi: 30 Mei 2025

Kwa wahitimu wanaotafuta nafasi ya kuanza safari yao ya kikazi katika mazingira ya kujifunza na kuleta mabadiliko kwenye jamii, hii ni fursa ya kipekee kutoka Ongeza Agrovet. Usikose nafasi hii – tuma maombi yako mapema!

Leave a Comment