Guides

Mfumo wa Maombi ya Kitambulisho cha Taifa Online – Jinsi ya Kujiandikisha

MFUMO wa Maombi ya Kitambulisho cha Taifa Online

Jinsi ya Kuomba Kitambulisho cha Taifa Kupitia Mtandao

Huduma hii ya mtandaoni imebuniwa kwa ajili ya kuwawezesha wananchi wa Tanzania – raia au wageni wakazi – kuwasilisha maombi ya Kitambulisho cha Taifa wakiwa mahali popote walipo. Mwombaji hujaza fomu ya maombi kwa njia ya kielektroniki kupitia mfumo wa NIDA, kisha kuichapisha na kuiwasilisha kwenye ofisi ya NIDA ya wilaya aliko kwa ajili ya hatua za mwisho za usajili wa alama za kibaiolojia (biometria).

Vielelezo Muhimu kwa Raia Anayeomba Kitambulisho cha Taifa

  • Cheti cha kuzaliwa cha mwombaji
  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa au kiapo cha mzazi mmoja
  • Kwa uraia wa kurithi: nakala ya cheti cha mzazi au kitambulisho cha Taifa cha mzazi
  • Kwa uraia wa kujiandikisha: nakala ya hati ya uraia (Dossier Number)

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kujaza Fomu ya Maombi

  • Kuwa na anwani sahihi ya barua pepe kwa ajili ya kujisajili na kupokea kiunga cha usajili
  • Kuwa na nyaraka mbili au zaidi za utambulisho kama vile cheti cha kuzaliwa
  • Kufanya “scanning” ya nyaraka zote na kuziweka katika mfumo wa PDF (ukurasa mmoja tu kwa kila kiambatisho), JPG au PNG
  • Kutoa namba ya simu ya mkononi
  • Waombaji waliozaliwa kuanzia 1980 wanatakiwa kuambatisha cheti cha kuzaliwa; waliozaliwa kabla ya hapo wanaweza kutumia cheti au kiapo cha kuzaliwa (Affidavit)
  • Kama una majina mengine, yafahamishe mapema kwa ajili ya marekebisho ya baadaye
  • Kujua majina ya wazazi wote wawili
  • Ikiwezekana, jumuisha Namba za Utambulisho (NIN) za wazazi
  • Eleza kwa usahihi anuani yako – namba ya nyumba, mtaa, na kata
  • Watanzania walioko nje ya nchi wanapaswa kupata uthibitisho wa makazi kutoka kwa afisa wa ubalozi wa Tanzania
  • Ambatisha nyaraka nyingine kama vyeti vya shule, namba ya mlipa kodi (TIN), na kadi ya mpiga kura
  • Hakikisha taarifa zote katika fomu zinawiana na nyaraka zako rasmi
  • Baada ya kujaza, fomu inapaswa kugongwa mhuri na kutiwa saini na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa unaoishi

Hatua ya Mwisho ya Uwasilishaji

Baada ya hatua zote, mwombaji anatakiwa kufika katika ofisi ya NIDA ya wilaya akiwa na fomu iliyokamilika pamoja na nakala halisi za vielelezo alivyowasilisha mtandaoni kwa ajili ya kukamilisha usajili. Kwa maelezo zaidi, unaweza kufika kwenye ofisi yoyote ya NIDA iliyo karibu nawe.

Anza Sasa

Kwa kuanza mchakato wa kujiandikisha kwa njia ya mtandao, bofya hapa:

Kujiandilisha bonyeza HAPA

Leave a Comment