Ajira Tanzania

Nafasi 694 za Kazi za Walimu wa Kujitolea Shule za Msingi Tamisemi

Nafasi 694 za Kazi za Walimu wa Kujitolea Shule za Msingi Tamisemi

Nafasi 694 za Kazi kwa Walimu wa Kujitolea Shule za Msingi Zatangazwa

Mradi wa Kuboresha Kada ya Ualimu (GPE – TSP) unaoendeshwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI umetangaza fursa 694 za kazi kwa walimu wa kujitolea katika shule za msingi. Nafasi hizi ni sehemu ya mkakati wa kuongeza nguvu kazi ya walimu kupitia mpango wa Primary Teacher Allocation Protocol (P-TAP), kwa lengo la kusaidia shule zenye uhitaji mkubwa zaidi wa walimu.

Walimu waliomaliza mafunzo yao katika vyuo vinavyotambulika na serikali wanahimizwa kutuma maombi kupitia mfumo wa kidigitali wa Online Teachers Application System (OTEAS) kwa kutumia tovuti ya ajira.tamisemi.go.tz kuanzia tarehe 17 Mei hadi 30 Mei 2025.

Nafasi Zinazopatikana

Nafasi hizo zinahusu walimu wa ngazi ya Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma) waliomaliza mafunzo yao kati ya mwaka 2015 hadi 2023.

Taratibu za Kuomba

Waombaji wote wenye sifa wanapaswa kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya ajira.tamisemi.go.tz kabla ya tarehe ya mwisho.

Sifa za Kitaaluma

  • Mwalimu Daraja III A: Astashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi
  • Mwalimu Daraja III B: Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali
  • Mwalimu Daraja III B: Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  • Awe raia wa Tanzania
  • Umri usiozidi miaka 43
  • Awe hajawahi kuajiriwa serikalini au kufukuzwa kwa makosa ya kiutumishi
  • Awe tayari kufanya kazi katika maeneo ya pembezoni yenye uhitaji mkubwa
  • Awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
  • Aambatishe vyeti vya kuzaliwa, elimu ya sekondari, na mafunzo ya ualimu
  • Waliosoma sekondari nje ya nchi wawe na Namba ya Ulinganifu (EQ) kutoka NECTA

Kwa maelezo zaidi kuhusu sifa na namna ya kutuma maombi, tembelea tovuti rasmi ya ajira TAMISEMI au wasiliana na huduma kwa wateja kwa namba: 026 2160210 au 0735 160210.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Mei 2025, saa 11:59 jioni.

Leave a Comment