Tetesi Mpya za Usajili Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2025/2026

0

Fahamu tetesi za usajili Ligi Kuu NBC 2025/2026, Simba, Yanga, Azam FC na vilabu vingine. Angalia orodha ya wachezaji wanaohusishwa.

Usajili Dirisha Dogo NBC 2025/2026: Nini Kinaendelea?

Msimu wa dirisha dogo la usajili kwa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kufunguliwa Januari 2025. Tayari vilabu vikubwa kama Simba, Yanga na Azam FC vinaingia sokoni kuhakikisha vikosi vyao vinaimarika kabla ya nusu ya pili ya msimu wa 2025/2026.

Timu Zaanza Kuwinda Wachezaji Kabla ya Dirisha Dogo

Baada ya mechi kadhaa za Ligi Kuu kupigwa, makocha wengi sasa wanaelewa maeneo ya kuimarisha na wachezaji wanaofaa kuongezwa au kuachwa. Makala hii inakuletea tetesi moto za usajili kutoka klabu mbalimbali.

Muhtasari wa Msimamo wa Ligi Kuu NBC

Msimu uliopita, Yanga ilitwaa ubingwa kwa pointi 80, ikifuatiwa na Azam FC na Simba SC ambazo zilimaliza na pointi 69 kila moja, Azam ikiwazidi Simba kwa tofauti ya magoli.

Tetesi za Usajili Simba SC 2025/2026

Simba SC inahusishwa na wachezaji kadhaa kuelekea dirisha dogo Januari 2025. Klabu hiyo ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwa pointi 28 baada ya mechi 11.

Wachezaji wanaohusishwa na Simba SC:

  • Foday Trawally
  • Abdelhay Forsy
  • Sabri Kondo
  • Charles Senfuko
  • Kambou Dramane
  • Lameck Elias Lawi
  • Ibrahima Seck
  • Allan Okello
  • Lasinne Kouma

Wachezaji wanaotarajiwa kuachwa:

  • Fabrice Ngoma
  • Ayoub Lakred

Tetesi za Usajili Yanga SC 2025/2026

Yanga SC ina mpango wa kuwaongezea mikataba wachezaji muhimu kama Salum Abubakar, Jonas Mkude, Bakari Mwamnyeto na Kibwana Shomari. Pia klabu inawania wachezaji wapya kadhaa.

Majina yanayohusishwa na Yanga:

  • Kelvin Nashon
  • Harvey Onoya (DRC)
  • Bruno Gomez (kurejea)
  • Fredy Michael Koublan
  • Lameck Lawi
  • Abdallah Said Lanso (KMC)
  • Mamadou Koita (Mali)
  • Jonathan Ikangalombo (AS Vita)
  • Kevin Nashon
  • Israel Mwenda
  • Micky Harvey Ossete
  • Lauren Makame

Taarifa nyingine:

  • Kibwana Shomari anahusishwa na mkopo kwenda KMC
  • Fahad Bayo (Uganda) anawindwa na Yanga
  • Kocha mpya msaidizi: Abdelhamid Moalin
  • Mtifuano unaendelea kati ya kocha Gamondi na baadhi ya wachezaji
  • CEO wa Yanga Andre Mtine na mwanasheria Simon Patrick wapo hatarini kutimuliwa
  • Yanga inaweza kufanya biashara na Singida: Jonathan Sowah kujiunga Yanga, Kennedy Musonda kwenda Singida kwa mkopo

Tetesi za Usajili Azam FC 2025/2026

Azam FC imetangaza kuachana na Malickou Ndoye na inatazamiwa kuachana pia na:

  • Abdulai Idrisu
  • Issah Ndala
  • Ali Ahmada

Wachezaji wengine:

  • Mohamed Mustapha (kurejea Al-Merreikh baada ya mkopo)
  • Salim Mwalimu anatakiwa na Azam
  • Lasinne Kouma pia anahusishwa na Azam

Tetesi Nyingine za Usajili NBC 2025/2026

  • Hussein Masalanga: huru baada ya kuachana na Ihefu FC
  • Yona Amosi: anatafuta timu mpya baada ya kutoka Tanzania Prisons
  • Pamba Jiji: wanataka kumsajili kocha Goran Kopunovic
  • Mashujaa FC: mazungumzo na golikipa Erick Johora (alitoka Geita Gold)
  • Dodoma Jiji: wametuma ofa kwa Sebu Sebu
  • Geofrey Muha & Sebu Sebu Samsoni: wanawaniwa na KMC, Kengold na Tanzania Prisons
  • Jaff Kibaya: ameachana na Singida Black Stars
  • Larry Bwalya: anawindwa na Pamba Jiji na Singida
  • Bruno Gomez: anaweza kurejea Singida
  • Jonathan Sowah: tayari amesajiliwa na Singida Black Stars
  • Mashabiki wa Gamondi wajiandae kuhamia Singida

Vilabu vya Ligi Kuu Tanzania Bara vinaonekana kushika kasi katika kusuka upya vikosi vyao kabla ya dirisha dogo kufunguliwa. Mashabiki wana matarajio makubwa ya kuona wachezaji wapya watakaoweka ushindani mkali msimu wa 2025/2026. Endelea kutembelea tovuti yetu kwa habari zaidi za soka la ndani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here