Bei Ya Mafuta ya Petroli Tanzania, Mei 2025

0

Bei Ya Mafuta Petroli Tanzania, May 2025

EWURA imetangaza bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika kuanzia Jumatano tarehe 7 Mei 2025, zikionyesha mabadiliko mbalimbali kwa petroli, dizeli na mafuta ya taa.

Taarifa Rasmi kutoka EWURA Mei 2025

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli zitakazotumika kuanzia saa 6:01 usiku, tarehe 7 Mei 2025.

Bei za Rejareja kwa Mei 2025

Jedwali Na. 1 linaonesha bei kikomo za rejareja kwa mafuta ya petroli katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara (Shilingi kwa Lita).

Bei za Jumla kwa Mei 2025

Jedwali Na. 2 linaonesha bei kikomo za jumla kwa bidhaa hizo katika maeneo husika.

Bei kwa Maeneo Mengine

Bei za mafuta kwa maeneo mengine ya miji na mikoa mbalimbali zimo kwenye Jedwali Na. 3 lililotolewa na EWURA.

Mabadiliko ya Bei Duniani

Katika soko la kimataifa, bei za mafuta yaliyosafishwa (FOB) kutoka Uarabuni zimepungua kwa asilimia 5.22 (petroli), 5.21 (dizeli) na 5.08 (mafuta ya taa).

Gharama za Uagizaji Mei 2025

Gharama za kuagiza mafuta (premiums) Dar es Salaam zimepungua kwa 22.41% (petroli) na 4.78% (dizeli), huku hakuna mabadiliko kwa mafuta ya taa. Tanga hakuna mabadiliko yoyote, lakini Mtwara gharama zimepungua kwa 34.81%.

Mabadiliko ya Viwango vya Kubadilisha Fedha

Wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni umepungua kwa asilimia 1.20 kwa mwezi huu.

Maelekezo kwa Wafanyabiashara

Wafanyabiashara wote wanapaswa kuuza mafuta kwa bei zilizowekwa kwenye Jedwali Na. 2 na 3. Yeyote atakayekiuka agizo hili atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Maagizo Muhimu kutoka EWURA

  • Bei za mafuta zinapatikana bure kupitia 15200# kwa mitandao yote.
  • Bei hizi zinaongozwa na ushindani wa soko kulingana na Sheria ya Mafuta ya 2015.
  • Makampuni ya mafuta yanaweza kuuza kwa bei yoyote isiyozidi kikomo kilichoainishwa.
  • Vituo vya mafuta vinapaswa kuweka mabango yanayoonyesha wazi bei za mafuta.
  • Wateja wanahimizwa kununua mafuta kwenye vituo vyenye bei nafuu zaidi.
  • Vituo vinapaswa kutoa stakabadhi za EFPP, zitakazotumika kama vielelezo vya bei na ubora.

Tazama Bei Kikomo Mei 2025

Bei mpya za mafuta nchini Tanzania zitaanza kutumika rasmi Jumatano tarehe 7 Mei 2025.

DOWNLOAD: Bei Ya Mafuta Petroli Tanzania PDF FILE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here