MAJINA ya Waliotwa Mafunzo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 2025
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetangaza majina ya vijana 445 waliochaguliwa kujiunga na mafunzo rasmi ya Uaskari katika ngazi ya Konstebo kwa mwaka 2025. Mafunzo haya ni sehemu ya ajira serikalini kwa ajili ya kuongeza nguvu kazi kwenye idara muhimu ya uokoaji nchini.
Tarehe na Mahali pa Kuripoti
Walioteuliwa wanapaswa kuripoti Chuoni Chogo, Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga kati ya tarehe 16 hadi 18 Mei 2025. Muda wa mapokezi ni kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku kila siku. Mtu yeyote atakayeshindwa kuripoti ndani ya muda huo hatapokelewa, na nafasi yake itatolewa kwa mtu mwingine.
Maelekezo Muhimu kwa Washiriki
Wahitimu wote wanatakiwa:
- Kujigharamia usafiri, chakula, na malazi hadi watakapopokelewa rasmi.
- Kufika wakiwa na vyeti halisi vya masomo, taaluma, au ujuzi, pamoja na cheti cha kuzaliwa na kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA.
- Kwa waombaji wa nafasi za udereva, kuja na leseni hai.
- Kila cheti kiwe na nakala tatu, na majina kwenye vyeti vyote yawiane. Waliogushi nyaraka au kuwa na majina yanayotofautiana watarudishwa.
- Kupitia vipimo vya afya ya mwili, akili, na mimba kwa wanawake. Atakayegundulika kuwa na matatizo ya kiafya hataruhusiwa kuendelea na mafunzo.
Vifaa vya Kuja Navyo Chuoni
Wahusika wanapaswa kubeba:
- Mashuka mawili (rangi ya bluu)
- Mto mmoja na foronya mbili (rangi ya bluu)
- Chandarua cha duara (bluu)
- Ndoo ya plastiki ya lita 20
- Sahani na kikombe cha bati
- Fedha kwa matumizi binafsi
- Kadi ya bima ya afya (kwa waliyonayo)
Vifaa Vitakavyonunuliwa Chuoni
Baadhi ya vifaa vinapatikana dukani ndani ya chuo:
- Raba za michezo
- Fulana (T-shirt) za bluu
- Madaftari makubwa (counter books 4 quire – pcs 5)
- Vifaa vya michezo (track suit, bukta bluu, fulana)
- Kalamu
Tahadhari Kali kwa Walaghai
Yeyote atakayebainika kuwasilisha vyeti au nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua kali za kisheria, ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Orodha ya Majina ya Waliochaguliwa
Kwa majina kamili ya waliopata nafasi,