Nafasi za Kujiunga JWTZ 2025 – Sifa, Taaluma Zinazohitajika na Jinsi ya Kutuma Maombi

0
Nafasi za Kujiunga JWTZ 2025

NAFASI MPYA ZA KUJIUNGA NA JWTZ 2025 – ANGALIA SIFA NA JINSI YA KUTUMA MAOMBI

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza rasmi nafasi mpya kwa vijana wa Kitanzania kujiunga na jeshi hilo kwa mwaka 2025, likilenga watu wenye elimu ya Sekondari hadi Vyuo Vikuu pamoja na waliobobea katika taaluma adimu.

Sifa Za Mwombaji Kujiunga JWTZ 2025

Kila kijana anayetaka kujiunga na JWTZ anatakiwa kutimiza masharti yafuatayo:

  • Awe Mtanzania mwenye Kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA.
  • Awe na afya njema na akili timamu.
  • Awe na nidhamu nzuri na hajawahi kuhukumiwa au kufungwa kwa kosa la jinai.
  • Awe na vyeti halisi vya kuzaliwa, shule na taaluma.
  • Awe hajahudumu katika Polisi, Magereza, KMKM au chombo kingine cha ulinzi.
  • Awe amehitimu JKT kwa mujibu wa sheria au kwa mkataba wa kujitolea.
  • Umri wa Mwombaji:
    • Kidato cha Nne/Sita – ≤ miaka 24
    • Stashahada – ≤ miaka 26
    • Shahada ya Chuo Kikuu – ≤ miaka 27
    • Madaktari Bingwa – ≤ miaka 35

Taaluma Adimu Zenye Kipaumbele JWTZ 2025

Afya:

  • Madaktari Bingwa: Surgeon, Urologist, Radiologist, Psychiatrist, nk.
  • Tiba ya Binadamu, Meno, Mifugo, Biomedical Engineering, Radiographer, nk.

Uhandisi:

  • Electronic, Mechanical, Marine, Aeronautic, na Air Traffic Management.

Ufundi:

  • Aluminium Welding, Metal Fabrication.

Utaratibu wa Kutuma Maombi JWTZ 2025

Waombaji wote wanatakiwa:

  • Kuandika barua kwa mkono.
  • Kuambatanisha:
    • Nakala ya NIDA au Kitambulisho cha Taifa
    • Cheti cha kuzaliwa
    • Vyeti vya shule/chuo
    • Cheti cha kuhitimu JKT (kwa waliopitia JKT)
    • Nambari ya simu ya mkononi

Muda wa Kutuma Maombi: Kuanzia 01 Mei hadi 14 Mei 2025

📨 Anwani ya Kutuma Maombi

Mkuu wa Utumishi Jeshini,  
Makao Makuu ya Jeshi,
S.L.P 194,
DODOMA, Tanzania

DOWNLOAD PDF: Download Tangazo la Kujiunga JWTZ 2025

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here