Yanga SC vs KVZ FC: Matokeo ya Robo Fainali Kombe la Muungano 26 Aprili 2025
Robo Fainali ya Kombe la Muungano Yanga SC vs KVZ FC
Yanga SC itaingia dimbani dhidi ya KVZ FC katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Muungano 2025 utakaopigwa Jumamosi, tarehe 26 Aprili 2025.
Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, kuanzia saa 1:15 usiku, na unatarajiwa kuwa wa kusisimua huku mashabiki wa pande zote wakisubiri kuona nani ataingia nusu fainali.
Habari Web Blog itakuwa nawe bega kwa bega kukuletea taarifa zote muhimu kuanzia dakika ya kwanza hadi ya tisini, zikiwemo mabao, matukio ya papo kwa papo, na matokeo ya mwisho ya mchezo huo muhimu.
Kikosi cha Yanga SC kinaingia katika mchezo huu kikiwa na morali ya juu baada ya kampeni bora kwenye ligi, huku KVZ FC nao wakitafuta kufanya maajabu dhidi ya moja ya vilabu vikubwa zaidi nchini.
Usikose Matokeo na Taarifa Kamili
Fuatilia ukurasa huu tarehe 26 Aprili kwa taarifa LIVE za KVZ FC vs Yanga SC — kutoka mwanzo hadi mwisho wa mchezo, tukuletee kila tukio moja kwa moja kutoka Gombani.