Kocha wa Al Ahly Marcel Koller Apambana Kuvunja Rekodi ya Pitso Mosimane CAF 2025

0
Kocha wa Al Ahly Marcel Koller Apambana Kuvunja Rekodi ya Pitso Mosimane CAF 2025

Kocha wa Al Ahly Marcel Koller Afukuzia Rekodi Mpya Afrika

Muda mchache Kabla ya Mchezo wa Pili wa Nusu Fainali CAF

Zikiwa zimebaki saa chache kabla ya mchezo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Al Ahly na Mamelodi Sundowns, presha iko juu kwa kocha wa Al Ahly, Marcel Koller, ambaye ana nafasi ya kuingia kwenye historia ya soka la Afrika.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Afrika Kusini, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana, hivyo kila kitu kitamuliwa kwenye mchezo wa marudiano.

Marcel Koller Kufikia Rekodi ya Pitso Mosimane?

Iwapo Al Ahly itafuzu fainali, Marcel Koller atakuwa amefikia rekodi ya kocha wa zamani wa klabu hiyo, Pitso Mosimane, aliyeifikisha timu hiyo fainali mara tatu mfululizo (2020, 2021, na 2022). Mosimane pia alitwaa ubingwa mwaka 2020 na 2021.

Koller, raia wa Uswizi, ana nafasi ya kuandika historia mpya kwa kuwa kocha wa kwanza kutwaa mataji matatu mfululizo na kuweka rekodi ya kipekee kwa klabu ya Al Ahly, ambayo haijawahi kufanya hivyo tangu kuanzishwa kwake.

Changamoto ya Kuvunja Mwiko Dhidi ya Sundowns

Koller hajawahi kuifunga Mamelodi Sundowns tangu ajiunge na Al Ahly. Katika mechi tano walizokutana, amepata sare tatu na kupoteza mbili. Mchezo huu unampa nafasi ya kipekee ya kubadili historia hiyo mbaya.

Historia Fupi ya Marcel Koller

Koller alianza kazi ya ukocha nchini Uswizi ambako alifundisha vilabu kama FC Basel, Grasshopper, na FC Wil kabla ya kujiunga na Al Ahly mnamo Septemba 9, 2022.

Nusu Fainali Nyingine: Pyramids vs Orlando Pirates

Misri au Afrika Kusini: Nchi Ipi Itapeleka Timu Mbili Fainali?

Katika nusu fainali nyingine, Pyramids FC watakuwa nyumbani kuikabili Orlando Pirates ya Afrika Kusini, baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza.

Iwapo Al Ahly na Pyramids zitafuzu fainali, Misri itakuwa imetoa timu mbili kwenye fainali kwa mara ya pili katika historia, baada ya mara ya kwanza mwaka 2020 (Al Ahly vs Zamalek). Kwa upande wa Afrika Kusini, hii itakuwa mara ya kwanza iwapo Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates zitatinga hatua ya fainali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here