Tetesi Mpya za Usajili Barani Ulaya Leo: De Bruyne, Kudus, Joao Felix na Wengine
Aston Villa Wafanya Majadiliano Kuhusu Kevin De Bruyne
Aston Villa wamefanya mazungumzo ya ndani kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo mkongwe wa Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji, Kevin De Bruyne, mwenye umri wa miaka 33, ambaye anatarajiwa kuondoka Etihad Stadium msimu huu wa joto. (Chanzo: Sky Sports)
Leeds United Wamuweka Daniel Farke Rehani
Leeds United wanatafakari kumfuta kazi kocha wao Daniel Farke, licha ya kufanikisha kurejea kwenye Ligi Kuu ya England msimu ujao. (Chanzo: Mail)
Vilabu Vikubwa Vyamtaka Milos Kerkez
Liverpool, Real Madrid, na Manchester City wanaripotiwa kuwa katika mbio za kumsajili beki wa kushoto kutoka Bournemouth na timu ya taifa ya Hungary, Milos Kerkez, mwenye umri wa miaka 21. (Chanzo: Sky Sports)
Mastantuono Awaniawa na Vigogo
Manchester United, Chelsea, na Real Madrid wanapigania saini ya kiungo chipukizi wa River Plate na timu ya taifa ya Argentina, Franco Mastantuono, 17, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa cha pauni milioni 38. (Chanzo: Mail)
Matheus Cunha Awindwa na Klabu 5 za EPL
Arsenal, Aston Villa, na Manchester United ni miongoni mwa klabu tano za EPL zinazowania kumsajili mshambuliaji wa Wolves na timu ya taifa ya Brazil, Matheus Cunha, 25. (Chanzo: Sky Sports)
James McAtee Kuwaniwa na Forest na Leverkusen
Iwapo Manchester City watamsajili Morgan Gibbs-White au Florian Wirtz, basi klabu ya Nottingham Forest na Bayer Leverkusen zitalenga kumsajili kiungo wa City, James McAtee, mwenye umri wa miaka 22. (Chanzo: Telegraph)
Kudus Apigiwa Hesabu na Al-Nassr
Mohammed Kudus, winga wa West Ham na timu ya taifa ya Ghana mwenye umri wa miaka 24, anahusishwa na uhamisho kwenda klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia. (Chanzo: Guardian)
Raphinha Awekewa Dili Kubwa na Al-Hilal
Al-Hilal wametuma ofa ya pauni milioni 75 (sawa na $100m) kwa Barcelona ili kumnunua winga wa Brazil Raphinha, 28. Mkataba uliopendekezwa una thamani ya £151m kwa miaka minne. (Chanzo: Sport)
Joao Felix Kuwania Kurudi Benfica
Mshambuliaji wa Chelsea na Ureno, Joao Felix, 25, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo AC Milan, ameanza mazungumzo ya kurejea katika klabu yake ya zamani Benfica. (Chanzo: CaughtOffside)
Flick Karibu Kusaini Mkataba Mpya na Barcelona
Barcelona inaendelea na mazungumzo na kocha wao wa sasa, Hansi Flick, 60, kuhusu kuongeza mkataba hadi mwaka 2027. (Chanzo: Sky Germany)
Real Madrid Wakaribia Kumsaini Vinicius Jr Mpya
Mchezaji wa kimataifa wa Brazil, Vinicius Jr, 24, yupo kwenye hatua za mwisho kusaini mkataba mpya na klabu yake ya sasa Real Madrid. (Chanzo: Fabrizio Romano)
Arsenal Waendeleza Mbio za Martin Zubimendi
Licha ya kuhusishwa na Real Madrid, klabu ya Arsenal bado ina matumaini ya kumsajili kiungo wa kati wa Real Sociedad, Martin Zubimendi, mwenye umri wa miaka 26. (Chanzo: CaughtOffside)
Junior Firpo Karibu Kujiunga na Real Betis
Leeds United, ambayo ilifanikiwa kupanda daraja wiki hii, inaweza kumpoteza beki wa Jamhuri ya Dominika, Junior Firpo, 28, anayewindwa na klabu ya zamani Real Betis. (Chanzo: Todofichajes)