Tetesi za Soka – Arsenal na Real Madrid Waingia Sokoni

0
Tetesi za Soka - Arsenal na Real Madrid Waingia Sokoni

Tetesi za Soka Leo April 18, 2025

Arsenal Wamvizia Kingsley Coman wa Bayern Munich

Ripoti kutoka Ujerumani zinaeleza kuwa Arsenal wanafikiria kumsajili winga wa Bayern Munich, Kingsley Coman, ambaye ana umri wa miaka 28. Mfaransa huyo ameonyesha kiwango kizuri lakini huenda akawa katika mabadiliko msimu huu wa joto.

Haaland Kuvuta Nia ya Real Madrid

Florentino Perez, Rais wa Real Madrid, anaripotiwa kuwa na nia ya kumsajili Erling Haaland kutoka Manchester City. Mshambuliaji huyo wa Norway mwenye umri wa miaka 24 ameendelea kung’ara kwenye Ligi Kuu ya England, hali inayozidi kuwavutia vigogo hao wa Hispania.

Rayan Cherki Kuwindwa na Manchester United na Liverpool

Vyanzo vya karibu vinaripoti kuwa Manchester United na Liverpool wanapigania saini ya Rayan Cherki, mshambuliaji chipukizi wa Lyon mwenye umri wa miaka 21. Klabu hizo zinapanga kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.

United na Tottenham Wamtupia Jicho Kaua Santos

Klabu za Manchester United na Tottenham Hotspur zimekuwa kwenye mazungumzo na Eintracht Frankfurt kuhusu uwezekano wa kumsajili kipa wa Kibrazil, Kaua Santos mwenye umri wa miaka 22.

Chelsea Walitaka Kumsajili Van Dijk

Chelsea walijaribu kuwania saini ya beki nyota wa Liverpool, Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 33, kabla ya kuamua kusalia Anfield na kusaini mkataba mpya.

Joao Felix Aelekea Kuondoka Ulaya

Mshambuliaji wa Chelsea anayekipiga AC Milan kwa mkopo, Joao Felix, anatazamiwa kuhamia Saudi Arabia au kurejea Benfica ya Ureno msimu huu wa joto, kulingana na taarifa za hivi karibuni.

Liverpool Wamtaka Hugo Ekitike

Liverpool wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike, raia wa Ufaransa mwenye miaka 22, kama sehemu ya kuimarisha safu ya ushambuliaji.

Everton vs Inter Milan kwa Albert Gudmundsson

Kiungo wa kati wa Genoa, Albert Gudmundsson, anayekipiga kwa mkopo Fiorentina, anawaniwa na Everton pamoja na Inter Milan. Raia huyo wa Iceland ana miaka 27 na amekuwa akionyesha kiwango bora.

Ancelotti Karibu na Kuondoka Real Madrid

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, mwenye miaka 65, anatazamiwa kuondoka baada ya fainali ya Copa del Rey dhidi ya Barcelona. Timu ya taifa ya Brazil inatajwa kuwa na nia ya kumteua kuwa kocha wao mpya.

Hudson-Odoi Karibu Kubaki Nottingham Forest

Nottingham Forest wameonyesha nia ya kumuongeza mkataba mpya Callum Hudson-Odoi, winga wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24, baada ya kuonyesha uwezo mzuri tangu ajiunge na klabu hiyo.

Barcelona Wajitoa kwa Nico Williams

Barcelona hawatashiriki tena katika mbio za kumsajili Nico Williams, winga wa Athletic Bilbao mwenye umri wa miaka 22, kwa mujibu wa gazeti la Marca.

Rodriguez Avutia Vilabu Vikubwa

Arsenal, Liverpool na Chelsea wapo mstari wa mbele kumnasa Jesus Rodriguez, kinda wa miaka 19 anayekipiga Real Betis. Nyota huyo wa Uhispania chini ya miaka 21 anaonekana kuwa na mustakabali mzuri.

Garnacho Kuwindwa na Atletico Madrid

Atletico Madrid wanaonyesha nia ya kumsajili Alejandro Garnacho wa Manchester United kwa dau la pauni milioni 70. Bayer Leverkusen pia wako kwenye kinyang’anyiro hicho kwa kijana huyo wa miaka 20 kutoka Argentina.

Gibril Sima Atazamwa na Tottenham

Mshambuliaji kijana kutoka Gambia, Gibril Sima mwenye miaka 17, anayekipiga Dutch Lions, ameanza kufuatiliwa na vilabu kadhaa ikiwemo Tottenham Hotspur.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here