Ratiba ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CRDB 2024/2025

0
Ratiba Rasmi ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CRDB

RATIBA ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CRDB

Hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho linalodhaminiwa na CRDB kwa msimu wa 2024/2025 imepangwa kufanyika katika mikoa ya Manyara na Tanga, ambapo timu nne zimefuzu kuwania nafasi ya kucheza fainali ya mashindano hayo makubwa ya kitaifa.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), mchezo mkali baina ya Yanga SC na JKT Tanzania utachezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, uliopo Jijini Tanga. Huu ni uwanja ambao mara kadhaa Yanga wamekuwa na rekodi nzuri, jambo linalowapa matumaini makubwa ya kusonga mbele.

Katika upande mwingine wa nusu fainali, timu ya Simba SC itavaana na Singida Black Stars katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo mkoani Manyara. Huu utakuwa mtihani mgumu kwa pande zote mbili, huku kila moja ikisaka tiketi ya kuingia fainali na kutwaa kombe.

Mechi hizi mbili zinatarajiwa kuchezwa kati ya tarehe 16 hadi 18 Mei, 2025, kipindi ambacho mashabiki wa soka nchini watakuwa macho kushuhudia burudani ya kiwango cha juu kutoka kwa vigogo wa soka la Tanzania.

Mashindano haya ya Kombe la Shirikisho la CRDB ni sehemu muhimu ya kalenda ya soka la Tanzania, yakitoa fursa kwa timu kuonyesha uwezo wao na kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kupitia ubingwa wa kombe hilo.

TFF imesisitiza kuwa maandalizi yote ya kiufundi na kiusalama yako tayari kuhakikisha michezo hiyo inachezwa katika mazingira salama na yenye ushindani wa haki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here