Safari za Treni ya Umeme SGR Dar hadi Dodoma Zimeanza Rasmi
Treni ya umeme ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma imeanza rasmi kutoa huduma, ikiwapa wasafiri nafasi ya kufurahia safari za haraka na za kisasa. Huduma hii mpya inajulikana kama “express train,” ikiwaleta wasafiri Dodoma kwa muda mfupi zaidi huku wakifurahia huduma za kipekee ndani ya treni.
Ratiba ya Safari na Vituo
Treni ya umeme ya SGR inaanza safari zake rasmi Julai 25, 2024. Treni inatoka Dar es Salaam saa 12:00 asubuhi na kufika Dodoma saa 3:25 usiku, ikichukua saa tatu na dakika 25 pekee. Treni itasimama Morogoro kabla ya kufika Dodoma. Kwa wasafiri wanaotumia treni ya kawaida, safari itaanza saa 3:30 asubuhi kutoka Dar es Salaam na kufika Dodoma baada ya kusimama kwenye vituo vidogo kama Pugu.
Nauli ya Treni ya Umeme ya SGR
Nauli zinatofautiana kulingana na aina ya treni na daraja la huduma:
Treni ya Kawaida:
- Tsh 31,000 kwa safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.
Treni ya Haraka (Express Train):
- Daraja la Biashara: Tsh 70,000
- Daraja la Juu: Tsh 120,000
Bei ya Tiketi Treni ya Mwendokasi SGR 2024 Kwa Abiria Wenye umri zaidi ya miaka 12
Bei ya Tiketi za Treni Ya Mwendokasi kwa daraja la kawaida kulingana na umbali wa vituo kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora kwa watu wazima na watoto wenye umri zaidi ya miaka 12 ni kama ifuatavyo;
Safari | Vituo | Umbali (Km) | Nauli (Shilingi) |
---|---|---|---|
Kutoka | Kwenda | Daraja la Kawaida | |
Dar es Salaam | Pugu | 19 | 1000 |
Dar es Salaam | Soga | 51 | 4000 |
Dar es Salaam | Ruvu | 73 | 5000 |
Dar es Salaam | Ngerengere | 134.5 | 9000 |
Dar es Salaam | Morogoro | 192 | 13000 |
Dar es Salaam | Mkata | 229 | 16000 |
Dar es Salaam | Kilosa | 265 | 18000 |
Dar es Salaam | Kidete | 312 | 22000 |
Dar es Salaam | Gulwe | 354.7 | 25000 |
Dar es Salaam | Igandu | 387.5 | 27000 |
Dar es Salaam | Dodoma | 444 | 31000 |
Dar es Salaam | Bahi | 501.6 | 35000 |
Dar es Salaam | Makutupora | 531 | 37000 |
Bei Ya Tiketi Kwa Abiria Wenye umri Kuanzaia Miaka 4 hadi 12
Aidha, mchanganuo wa Bei ya tiketi za Treni ya mwendokasi kwa daraja la kawaida kulingana na umbali wa vituo kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora kwa watoto wenye umri kuanzia miaka minne (4) hadi 12 ni kama ifuatavyo;
Safari | Vituo | Umbali (Km) | Nauli (Shilingi) |
---|---|---|---|
Kutoka | Kwenda | Daraja la Kawaida | |
Dar es Salaam | Pugu | 19 | 500 |
Dar es Salaam | Soga | 51 | 2000 |
Dar es Salaam | Ruvu | 73 | 2500 |
Dar es Salaam | Ngerengere | 134.5 | 4500 |
Dar es Salaam | Morogoro | 192 | 6500 |
Dar es Salaam | Mkata | 229 | 8000 |
Dar es Salaam | Kilosa | 265 | 9000 |
Dar es Salaam | Kidete | 312 | 11000 |
Dar es Salaam | Gulwe | 354.7 | 12500 |
Dar es Salaam | Igandu | 387.5 | 13500 |
Dar es Salaam | Dodoma | 444 | 15500 |
Dar es Salaam | Bahi | 501.6 | 17500 |
Dar es Salaam | Makutupora | 531 | 18500 |
Upatikanaji wa Tiketi
Tiketi za treni zinapatikana kwa njia ya mtandao kupitia tovuti rasmi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na pia katika stesheni za SGR. Kwa muongozo wa jinsi ya kukata tiketi mtandaoni, tafadhali angalia chapisho letu, “Jinsi Ya kukata Tiketi Ya Treni Online.” Hii inawawezesha wasafiri kupanga safari kwa urahisi na kwa wakati wao, huku wakihakikisha wanapata tiketi mapema.
Leave a Comment