Ratiba ya Michuano ya CRDB Federation Cup 2024/2025
Ratiba ya CRDB Federation Cup 2025 – Mechi za Robo na Nusu Fainali. Michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara maarufu kama CRDB Federation Cup kwa msimu wa 2024/2025 inaendelea kushika kasi, huku mashabiki wakifuatilia kwa karibu maendeleo ya timu zao pendwa. Katika raundi ya nne ya mashindano haya, timu kutoka ligi mbalimbali nchini zimeshiriki, zikiwemo za Ligi Kuu Tanzania Bara (PL), Championship League (CL), First League (FL), pamoja na Regional Championship League (RCL).
Ratiba ya Robo fainali Kombe la Shirikisho la CRDB 2024/25
Jumanne, Aprili 15 | Saa 10:00 Jioni
Yanga SC vs Stand United
Ratiba ya Nusu Fainali ya CRDB Federation Cup 2024/2025
Young Africans/Stand United | VS | JKT Tanzania |
Simba SC | VS | Singida Big Stars |
Mechi hizi za nusu fainali zinatarajiwa kuwa za aina yake, hasa ikizingatiwa uwezekano wa kuwepo kwa mechi kati ya watani wa jadi, Simba SC na Yanga SC, endapo Yanga wataibuka na ushindi dhidi ya Stand United. Hali hii inazidi kuongeza mvuto wa mashindano, huku kila timu ikitafuta nafasi ya kushinda taji la msimu huu wa CRDB Federation Cup.
Katika hatua ya robo fainali, mechi ziliandaliwa kuchezwa kuanzia saa 10:00 jioni, isipokuwa pale panapotokea mabadiliko rasmi. Ratiba hii inaonesha matokeo ya hatua hiyo na kuonyesha mwelekeo wa mechi za nusu fainali zinazofuata.
Matokeo ya Robo Fainali ya CRDB Federation Cup 2024/2025
Jumapili, Aprili 13
Simba SC 3-1 Mbeya City
Jumatatu, Aprili 14
JKT Tanzania 3-1 Pamba Jiji
Singida Big Stars 2-0 Kagera Sugar
Jumanne, Aprili 15
Yanga SC vs Stand United (Mechi inatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni)
Mashindano haya yanaendelea kuonesha ushindani wa hali ya juu, huku timu kubwa zikitumia kila nafasi kuhakikisha zinatinga hatua ya fainali. Simba SC tayari imeonyesha ubabe kwa kuichapa Mbeya City kwa mabao 3-1, huku Singida Big Stars nao wakionesha makali yao dhidi ya Kagera Sugar. JKT Tanzania wameonesha uwezo wao kwa kuishinda Pamba Jiji kwa mabao 3-1.
Kwa sasa, macho na masikio ya mashabiki wote yanaelekezwa kwenye mechi ya Yanga SC dhidi ya Stand United, ambayo itaamua ni timu ipi itaungana na Simba, Singida Big Stars, na JKT Tanzania katika hatua ya nusu fainali.