Soka

Taifa Stars vs Guinea: Matokeo Kufuzu AFCON 2025

Taifa Stars vs Guinea Kufuzu AFCON 2025

Matokeo ya Mechi ya Taifa Stars Vs Guinea Leo

Leo, timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imepambana na Guinea katika mechi muhimu ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Mchezo huu umefanyika kwenye Uwanja wa Charles Konan Banny, Yamoussoukro, Ivory Coast. Taifa Stars imeingia uwanjani kutafuta ushindi baada ya sare tasa kwenye mechi ya awali dhidi ya Ethiopia.

Matokeo ya Mechi ya Taifa Stars Vs Guinea

Guinea1 – 2Tanzania

Safu ya Ushambuliaji ya Taifa Stars na Changamoto Zake

Katika mchezo wa leo, safu ya ushambuliaji ya Taifa Stars iliongozwa na Wazir Junior na Cyprian Kachwele, wakisaidiana na Simon Msuva katikati. Hata hivyo, changamoto imeendelea kuwa kwenye utumiaji wa nafasi nyingi zinazotengenezwa bila kuzitumia ipasavyo.

Guinea na Presha ya Kujiimarisha

Guinea iliingia kwenye mchezo huu ikitafuta kurejesha heshima baada ya kipigo cha 1-0 dhidi ya DR Congo kwenye mechi ya awali. Timu hiyo imekuwa ikisuasua baada ya ushindi mfululizo mwezi Machi na Juni, na presha ilikuwa juu kurekebisha mwenendo mbovu wa kufungwa.

Matokeo ya Mechi na Muda Muhimu

  • Matokeo: Guinea 1-2 Tanzania
  • 57′ Guinea ilitangulia kwa goli la kwanza.
  • 61′ Feisal Salum alisawazisha kwa Tanzania.

Kikosi cha Taifa Stars

  • Mchezaji wa Golini: Ally Salum
  • Mabeki: Lusijo Mwaikenda, Mohamed Hussein (C), Dickson Job, Ibrahim Abdilla
  • Viungo: Novatus Dismas, Edwin Balama, Mudathir Yahya, Feisal Salum
  • Washambuliaji: Walid Junior, Wazir Junior
  • Kocha: Hemed Morocco

Rekodi za Taifa Stars Mwaka 2024

Kwa mwaka 2024, Taifa Stars imekuwa na changamoto nyingi, ikishinda mechi tatu pekee kati ya 11 zilizochezwa. Ushindi wa hivi karibuni dhidi ya Zambia uliwapa mashabiki matumaini makubwa, huku safu ya ulinzi ikionyesha uimara kwa kupata clean sheet sita katika mechi hizo.

Msimamo wa Kundi H na Matumaini ya Kufuzu AFCON 2025

Katika kundi H, Taifa Stars, Guinea, DR Congo, na Ethiopia zinachuana vikali kufuzu AFCON 2025. Kabla ya mechi ya leo, DR Congo ilikuwa ikiongoza kundi hilo na pointi tatu. Ushindi leo ungekuwa muhimu kwa Tanzania kuweka hai matumaini ya kufuzu michuano inayotarajiwa kufanyika Morocco kuanzia Desemba 21, 2025.

Leave a Comment