Jinsi Ya

Jinsi ya Kupiga Kura Tuzo za Muziki TMA 2024

Jinsi ya Kupiga Kura Tuzo za Muziki TMA 2024

Mwongozo Kamili wa Kupiga Kura Tuzo za Muziki Tanzania TMA 2024

Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) ni sherehe ya kipekee inayotambua vipaji vya muziki nchini Tanzania. Mwaka 2024, tuzo hizi zinaleta ushindani mkali kati ya wasanii maarufu kama Alikiba, Diamond Platnumz, Zuchu, na Nandy. Hafla hii ya kihistoria itafanyika Septemba 29, 2024, na wadhamini wakuu ni Pepsi pamoja na ushirikiano kutoka MTV Africa na BET.

Njia za Kupiga Kura

Mashabiki wanaweza kupiga kura kwa wasanii wao wapendwa kwa njia mbili:

  1. Kupiga Kura Mtandaoni:
    • Tembelea tovuti rasmi ya TMA 2024: tanzaniamusicawards.com.
    • Fuata maelekezo na chagua mteule wako kutoka kwenye makundi.
    • Thibitisha uchaguzi wako kulingana na maelekezo.
  2. Kupiga Kura kwa SMS:
    • Tuma namba ya mteule uliyemchagua kwenda namba 0738259611.

Kura zitafungwa Septemba 28, 2024, hivyo ni muhimu kupiga kura mapema.

Tarehe Muhimu na Vidokezo:

  • Kura zinaanza rasmi Septemba 4, 2024.
  • Hakikisha unatumia namba sahihi ya mteule ili kura yako ihesabiwe kwa usahihi.

Vipengele na Wasanii Watakaowania Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2024

Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2024 imeleta vipengele mbalimbali ambavyo vinashindanisha wasanii bora wa muziki wa Tanzania. Hivi hapa ni vipengele na wasanii wanaoshindania tuzo katika kila kipengele:

1. Mwanamuziki Bora wa Kiume wa Mwaka

  • Marioo – “Shisha”
  • Diamond Platnumz – “Shu”
  • Harmonize – “Single Again”
  • Alikiba – “Sumu”
  • Jay Melody – “Nitasema”

2. Mwimbaji Bora wa Kiume wa Bongo Fleva wa Mwaka

  • Diamond Platnumz – “Yatapita”
  • Jay Melody – “Sawa”
  • Alikiba – “Mahaba”
  • Marioo – “Love Song”
  • Harmonize – “Single Again”

3. Mwimbaji Bora wa Kike wa Bongo Fleva wa Mwaka

  • Zuchu – “Naringa”
  • Appy – “Watu Feki”
  • Nandy – “Falling”
  • Phina – “Sisi Ni Wale”
  • Anjella – “Blessing”

4. Wimbo Bora wa Ushirikiano wa Mwaka

  • Alikiba ft Marioo – “Sumu”
  • Mbosso ft Chley – “Sele”
  • Abigail Chams ft Marioo – “Nani”
  • Jux ft Diamond Platnumz – “Enjoy”
  • Diamond Platnumz ft Koffie Olomide – “Achii”

5. Albumu Bora ya Mwaka

  • Abigail Chams – “5”
  • D Voice – “Swahili Kid”
  • Navy Kenzo – “Most People Want This”
  • Harmonize – “Visit Bongo”
  • Rayvanny – “Flowers III”

6. Mwanamuziki Bora Chipukizi wa Mwaka

  • Xouh – “Lalala”
  • Chino Kidd – “Gibela”
  • Appy – “Watu Feki”
  • Mocco Genius – “Mi Nawe”
  • Yammi – “Namchukia”

7. Wimbo Bora wa Hip Hop wa Mwaka

  • Rapcha – “Uongo”
  • Country Wizzy – “Current Situation”
  • Young Lunya – “Stupid”
  • Stamina ft Bushoke – “Machozi”
  • Joh Makini – “Bobea”

8. Mwimbaji Bora wa Hip Hop wa Mwaka

  • Young Lunya – “Stupid”
  • Kontawa – “Dunga Mawe”
  • Stamina – “Machozi”
  • Joh Makini – “Bobea”
  • Rosa Ree – “Mama Omollo”

9. Mtumbuizaji Bora wa Kike wa Mwaka

  • Zuchu – “Nani Remix”
  • Phina – “Do Salale”
  • Abigail Chams – “Milele”
  • Da Princess – “Lolo”

10. Mtumbuizaji Bora wa Kiume wa Mwaka

  • Mbosso – “Sele”
  • Christian Bella – “Tamu”
  • Harmonize – “Single Again”
  • Alikiba – “Sumu”
  • Diamond Platnumz – “Shu!”

11. Mwimbaji Bora wa Muziki wa Dansi wa Mwaka

  • Christian Bella – “Kanivuruga”
  • Melody Mbassa – “Hellena”
  • Papi Kocha – “Jela ya Mapenzi”
  • Charlz Baba – “Mmbeya”
  • Sarah Masauti – “Popo”

12. Wimbo Bora wa Asili wa Mwaka

  • Sinaubi – “Pesa”
  • Man Fongo & Nyati Group – “Sauti ya Kumoyo”
  • Erica Lilakwa – “Aragoba”
  • Wazawa Music Band – “Muziki Hauna Mwenyewe”
  • Wamwiduka Band – “Usizime Muziki”

13. Mwanamuziki Bora wa Nyimbo za Asili

  • Elizabeth Maliganya – “Boda Boda”
  • Erica Lulakwa – “Aragoba”
  • Sinaubi Zawose – “Pesa”
  • Ngapi Group – “Berita”
  • Wamwiduka Band – “Usizime Muziki”

14. Mwimbaji Bora wa Muziki wa Taarabu wa Mwaka

  • Salha – “DSM Sweetheart”
  • Mwinyimkuu – “Bila Yeye Sijiwezi”
  • Malkia Leyla Rashid – “Watu na Viatu”
  • Amina Kidevu – “Hatuachani”
  • Mwansiti Mbwana – “Sina Wema”

15. Wimbo Bora wa Reggae wa Mwaka

  • Warriors From The East – “Wewe”
  • Akilimali – “Africa Mama”
  • Dimateo Zion – “Rhymes ToNight”
  • Mr. Kamanzi – “Give And Thanks”
  • Paul Mihambo – “Salamu Zako”

16. Mwanamuziki Bora wa Dancehall wa Mwaka

  • Dj Davizo – “Dancehall”
  • Baddest 47 – “Zagamua”
  • Appy – “Mr Hater”
  • Bayo The Great – “Nakupenda”

17. Video Bora ya Muziki wa Mwaka

  • Billnass – “Maokoto”
  • Mbosso – “Sele”
  • Zuchu ft Innos B – “Nani Remix”
  • Diamond Platnumz ft Koffie Olomide – “Achii”

Soma: Jinsi Ya Kuangalia Taarifa Zangu Za Nida PDF 2024

Vipengele hivi vinawapa wasanii nafasi ya kutambuliwa kwa kazi zao bora na mashabiki wanaweza kupiga kura kuamua nani atashinda katika kila kipengele.

Leave a Comment