Soka

Wafungaji Vinara Ligi Kuu NBC Tanzania 2024/2025

Wafungaji Vinara Ligi Kuu NBC Tanzania 2024/2025

Orodha ya wafungaji vinara NBC Premier League 2024/25. Je, Aziz Ki atatetea kiatu chake cha dhahabu, au kuna nyota mpya anayeng’ara?

Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2024/2025 | Vinara wa Magoli NBC Premier league 2024-25

Vinara wa Magoli Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2024/2025 wameanza kujitokeza katika msimu huu wa kusisimua wa NBC Premier League. Ligi hii maarufu inahusisha timu bora kutoka pande zote za Tanzania, zikijitahidi kuonyesha ubora wao uwanjani kwa lengo la kumaliza msimu wakiwa mabingwa. Yanga SC, mabingwa watetezi, wanajitahidi kutetea taji lao huku mchezaji wao mahiri, Stephan Aziz Ki, akitarajia kulinda kiatu chake cha dhahabu baada ya kufunga magoli 21 msimu uliopita.

Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania

Katika kila msimu wa Ligi Kuu ya NBC, mashindano ya kuwania kiatu cha dhahabu huleta msisimko mkubwa kwa mashabiki na wachezaji. Msimu huu wa 2024/2025 unaonekana kuwa na ushindani wa hali ya juu, huku wachezaji mbalimbali wakijitahidi kutikisa nyavu na kuongeza idadi ya mabao yao. Hadi sasa, tumeshuhudia wachezaji kadhaa wakifanya vizuri na kuweka majina yao katika orodha ya vinara wa magoli.

Orodha ya Wafungaji Vinara wa NBC Premier League 2024/2025:

  1. Valentino Mashaka – Simba SC – 2 Magoli
  2. Emmanuel Keyekeh – Singida BS – 1 Goli
  3. Jean Ahoua – Simba SC – 1 Goli
  4. Steven Mukwala – Simba SC – 1 Goli
  5. Salum Chuku – Tabora United – 1 Goli
  6. Anthony Tra Bi – Singida BS – 1 Goli
  7. Heririer Makambo – Tabora United – 1 Goli
  8. Che Malone Fondoh – Simba SC – 1 Goli
  9. Djuma Shabani – Namungo FC – 1 Goli
  10. Awesu Awesu – Simba SC – 1 Goli

Msimu huu wa 2024/2025 bado unaendelea, na orodha ya wafungaji bora ina nafasi kubwa ya kubadilika. Wachezaji wanaendelea kujituma kwa bidii ili kuimarisha nafasi zao katika mbio za kuwania kiatu cha mfungaji bora. Mashabiki wanatazama kwa hamu kubwa kuona nani ataibuka kidedea mwishoni mwa msimu huu, na iwapo Stephan Aziz Ki ataweza kutetea nafasi yake kama mfungaji bora, au kama kuna nyota mpya atakayeng’ara msimu huu.

Leave a Comment